01 / Maswali
Maswali yanayoulizwa.
Majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Mko wapi?
Showroom yetu iko Mwenge Mpakani, Dar es Salaam.
Njia gani za malipo mnapokea?
Tunapokea aina zote za malipo: fedha taslimu, malipo ya benki, na mobile money (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa).
Je, naweza kufanya test drive?
Ndiyo, test drive inawezekana. Karibu ofisini kwetu Mwenge Mpakani uone gari mwenyewe na ulijaribu.
Mnasaidia na usajili/nyaraka?
Ndiyo. Magari yetu yana karatasi zote na usajili upo.
Mnaleta magari mikoani?
Ndiyo, tunapeleka magari mikoani. Gharama ya usafirishaji inategemea umbali — wasiliana nasi tukueleze kwa mkoa wako.
Mnaagiza gari nisilolipata?
Ndiyo. Tunaagiza magari kutoka sehemu tofauti tofauti kutegemea aina ya gari unalolitaka. Tuambie unataka gari la aina gani au brand gani.
Mnafungua saa ngapi?
Tupo wazi saa 24, Jumatatu hadi Jumamosi. Karibu ofisini Mwenge Mpakani wakati wowote, au tupigie simu.
Mna dhamana (warranty)?
Ndiyo, tunatoa dhamana. Masharti yake yanategemea gari lenyewe — uliza ofisini kwa gari unalolitaka.
Naweza kubadilisha gari langu na lenu?
Ndiyo, tunabadilisha. Lete gari lako tuliangalie na tukupe thamani yake.
Mnanunua magari ya watu?
Ndiyo, tunanunua magari. Lete gari lako ofisini Mwenge Mpakani tuliangalie.
Naweza kulipa kidogo kidogo?
Ndiyo. Lipa nusu ya bei, beba gari, na salio ulipe kwa awamu. Masharti kamili ya mkopo utapewa na meneja.
Nikipata tatizo baada ya kununua?
Hakuna shida — wasiliana nasi moja kwa moja au fika ofisini Mwenge Mpakani tukusaidie.
Mnakodisha magari?
Ndiyo, tunakodisha magari kwa harusi, safari na matukio mengine. Bei inategemea gari lenyewe — tuambie tarehe na aina ya gari unayohitaji.